IQNA

Wanafunzi nchini Morocco

Wanafunzi nchini Morocco hawataki Mahusiano ya Kielimu na Israeli huku kukiwa Vita dhidi ya Gaza vikiendelea

13:00 - June 27, 2024
Habari ID: 3479023
IQNA-Ombi limetiwa saini na mamia ya wanafunzi na wahitimu katika chuo kikuu nchini Morocco, wakitaka kukatishwa kwa makubaliano ya ushirikiano na vyuo vikuu nane vya utawala haramu wa Israel.

Morocco, wakitaka kukatishwa kwa makubaliano ya ushirikiano na vyuo vikuu nane vya utawala haramu wa Israel.

 Ombi hilo, lililotiwa saini Jumatano na wanafunzi 1,256 na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mohammed VI Polytechnic katika mji wa kati wa Ben Guerir, lilitoa wito kwa utawala wa chuo kikuu "kukata uhusiano na washirika wa Israeli wanaohusika katika uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina," kulingana na kauli yao.

 Waliotia saini walisema kwamba walialikwa kwenye mazungumzo na walifanya mkutano na mwakilishi wa chuo kikuu, ambaye alionyesha kuwa chuo kikuu kinakataa kukata uhusiano na washirika wake wa Israeli.

 "Chuo kikuu chetu sio tu kimejishughulisha na urekebishaji lakini pia kimekuwa kinara katika kuanzisha mashirikiano na kukaribisha wajumbe wa ngazi za juu," ilisema taarifa hiyo.

 "Chuo kikuu kiliunda nafasi ya juu iliyojitolea kushughulikia ushirikiano wa Israeli, ambayo ni kitendo cha kipuuzi na uchochezi."

 Taarifa hiyo ilisema ushirikiano huo unahusisha vyuo vikuu nane vya Israeli na taasisi za elimu ya juu, ambazo zinajumuisha karibu vyuo vikuu vyote vya Israeli.

Ushirikiano unaozungumziwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Bar-Ilan, Chuo Kikuu cha Ben-Gurion, Chuo Kikuu cha Tel Aviv, Chuo cha Taaluma cha Western Galilee, Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Jerusalem, Taasisi ya Teknolojia ya Technion - Israel, Chuo Kikuu cha Reichman, na Chuo cha Sapir Academic, kulingana na taarifa hiyo.

 Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kukubali kurejesha uhusiano na utawala wa Israel mwaka 2020 baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan.

 Ikipuuza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano, Israel imekabiliwa na shutuma za kimataifa huku kukiwa na kuendelea na mashambulizi ya kikatili huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023.

 Raia wa Morocco Wasisitiza Wito wa Kukomesha Mauaji ya Kimbari ya Israel

Zaidi ya Wapalestina 37,700 wameuawa huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na karibu wengine 86,400 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.

 Zaidi ya miezi minane ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Ukanda wa Gaza yalikuwa magofu huku kukiwa na kizuizi cha chakula, maji safi na dawa.

 Utawala katili wa Israel unashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ambayo uamuzi wake wa hivi punde uliiamuru Tel Aviv kusitisha mara moja operesheni yake huko mjini Rafah Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni moja walitafuta hifadhi kutokana na vita kabla ya kuvamiwa Mei 6, 2024, mwaka huu.

 3488900

Kishikizo: morocco
captcha