IQNA

Nakala za Qur'ani zasambaziwa abiria katika Uwanja wa Ndege wa Al-Aaroui nchini Morocco

17:21 - July 26, 2025
Habari ID: 3480999
IQNA – Kwa lengo la kueneza mafundisho ya Uislamu, maafisa wa serikali ya Morocco wamegawa nakala za Qur’ani Tukufu kwa Wamorocco wanaoishi nje ya nchi waliporejea nyumbani.

Kwa mujibu wa taarifa ya News 55, katika kuadhimisha miaka 26 ya kuanza kwa uhusiano wa kindugu na mshikamano kati ya familia ya kifalme ya Alaouite na raia wa Morocco, Baraza la Wataalamu wa Kiislamu wa Mkoa wa Nador, kwa ushirikiano na Bodi ya Mambo ya Kiislamu ya kanda hiyo, waliandaa hafla maalum ya kuwapokea Wamorocco wanaorejea kutoka ughaibuni.

Hafla hiyo ilifanyika Jumatano jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al-Aaroui, mjini Nador.

Katika hafla hiyo, nakala za Qur’ani Tukufu ziligawiwa kwa raia hao waliorejea nyumbani, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuimarisha utambuzi wa kiroho na dini miongoni mwa Wamorocco wa Diaspora. Nakala hizo zilikuwepo kwa lugha ya Kiarabu, pamoja na tafsiri kwa Kifaransa na Kihispania—ili kurahisisha ufahamu wa mafundisho ya Kitabu hicho kitukufu kwa wale wanaoishi katika mataifa hayo.

Viongozi mashuhuri wa Kiislamu kutoka Morocco walihudhuria hafla hiyo, wakionyesha kuunga mkono juhudi hizi za kielimu na kiroho. Mpango huu unatekelezwa kama sehemu ya mkakati mpana wa kueneza dini na kuimarisha nafasi ya taasisi za kidini katika kuendeleza mawasiliano baina ya Morocco na raia wake walioko ughaibuni, hatua iliyopokelewa kwa furaha na jamii ya Wamorocco.

3493982

Kishikizo: qurani tukufu morocco
captcha