IQNA

Kanuni mpya zaibua changamoto katika mfumo wa elimu ya Qur'ani nchini Morocco

15:32 - May 05, 2025
Habari ID: 3480638
IQNA – Taasisi za elimu za kitamaduni nchini Morocco zimekumbana na changamoto baada ya kuwasilishwa kwa kanuni mpya za kusaidia vituo binafsi vya Qur'ani.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu imetangaza kanuni hizo mnamo Machi 18, kwa mujibu wa Madar24. Kitabu hicho cha kanuni kimeweka masharti magumu kwa shule na taasisi za elimu, ambazo zinapata ugumu kuyatekeleza, hasa katika maeneo yenye miundombinu duni na ukosefu wa vifaa.

Sharti mojawapo ni kwamba taasisi za elimu haziruhusiwi kupokea wanafunzi ambao hawajaorodheshwa katika ngazi za elimu rasmi. Hali hii ni changamoto kwani wanafunzi hao ndio nguzo kuu za kozi za kuhifadhi Qur'ani katika shule hizo.

Wanaharakati wa elimu wanaamini kwamba masharti haya yaliyotangazwa yataathiri vibaya elimu ya kitamaduni, ambayo ndiyo mhimili mkuu wa ufundishaji wa kuhifadhi Qur'ani.

Hasa, baadhi ya masharti haya yanasisitiza ujenzi wa majengo tofauti kulingana na makundi ya umri na ushirikiano na shule za jirani za Qur'ani, jambo ambalo ni gumu kufanikisha katika maeneo mengi ya mbali.

Pia, wachunguzi wanachukulia kuwa si haki kuunganisha msaada wa kifedha na idadi ya wanafunzi na matokeo ya kitaaluma, ikizingatiwa tofauti kubwa za rasilimali na uwezo kati ya taasisi moja na nyingine. Kinachozidisha hali ni muda mfupi uliotolewa kwa taasisi kufuata masharti mapya. Zinapaswa kutimiza masharti haya kufikia mwisho wa Mei 2025, hali inayoziacha shule kadhaa katika hatari ya kupoteza msaada au hata kufungwa kabisa.

Wanaharakati wa elimu wanasisitiza kuwa kutekeleza masharti haya bila mpangilio wa hatua kwa hatua au bila msaada wa wizara ya wakfu kunaweza kudhoofisha mfumo wa elimu ya kitamaduni na kuwanyima wanafunzi wengi fursa ya kupata elimu ndani ya mfumo wa elimu ya kidini ya asili na ya kitamaduni.

3492940

Kishikizo: morocco qurani tukufu
captcha