Siku ya kwanza baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa 14 wa rais wa Iran, Masoud Pezeshkian alitembelea kaburi la Imam Khomeini kusini mwa Tehran siku ya Jumamosi.
Baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Imam Khomeini (RA) na kusoma dua, alitoa hotuba ambapo alimshukuru Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei kwa kuandaa njia ya ushiriki mkubwa zaidi wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi na kuthamini ushiriki wa wananchi wa Iran kwa shauku katika uchaguzi.
Pia alisisitiza dhamira yake ya kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Daktari Massoud Pezeshkian alirejelea mauaji ya Ashura na kusema moja ya sababu kuu za yaliyotokea Karbala ni kwamba baadhi ya watu walitoa ahadi lakini wakashindwa kuzitekeleza.
Umuhimu wa Al-Wafa bil-Ahd (kutimiza ahadi za mtu) ni mojawapo ya mafunzo ya mauaji ya Ashura, aliongeza kwa kusema.
Pia alisema atatafuta kuendeleza mazungumzo, muunganiko, na makubaliano ya kitaifa, na akaapa kushughulikia matatizo ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kitamaduni na kisiasa.
Rais Mteule wa Iran Masoud Pezeshkian ni Nani?
Kwa jumla ya kura 30,530,157 zilizohesabiwa, Pezeshkian alipata kura nyingi zaidi kwa kupata kura 16,384,403, huku Jalili akipata kura 13,538,179.
Zaidi ya Wairani milioni 61 walistahili kupiga kura Ijumaa hii.
Na Hesabu ya kura ilianza mara tu baada ya kumalizika kwa upigaji kura, na kuhitimisha muda wa saa 16 wa upigaji kura ambao ulirekodi idadi ya wapigakura waliojitokeza kuwa asilimia 49.7, ambayo ilikuwa kubwa zaidi kuliko waliojitokeza kwenye uchaguzi wa Juni 28,2024 mwaka huu.
Daktari Massoud Pezeshkian alipata kura nyingi katika duru ya pili ya uchaguzi siku ya Ijumaa, na kuwa rais wa tisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.