Ali Reza Moaf, Mkuu wa Utafiti na Mipango katika Baraza la Kuratibu Maendeleo ya Kiislamu, aliyasema hayo katika mahojiano na IQNA kabla ya kumbukumbu ya mwaka wa 36 tangu kufariki kwa Imam Khomeini.
Amesema kwamba kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, kulikuwa na juhudi nyingi za kulisahaulisha suala la Palestina, lakini Imam Khomeini alizikomesha njama hizo.
Kwa mujibu wa Moaf, kwa kuanzisha Siku ya Kimataifa ya Quds, inayoadhimishwa Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani, na kupitia sera thabiti na endelevu ya Jamhuri ya Kiislamu kuhusu suala la Palestina na Quds, leo hii suala hilo limekuwa kipaumbele cha kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu.
Aidha, Moaf aligusia ibada ya Hija inayokuja na akaangazia mtazamo wa Imam Khomeini kuhusu umuhimu wa kisiasa wa Hija, akisema kuwa Imam Khomeini alieleza kwa kina upekee wa Hija kama jukwaa la kuonesha msimamo dhidi ya uonevu na dhulma.
“Ni muhimu kutumia msimu wa Hija kama chombo cha diplomasia ya umma ili kufichua sura halisi ya haki za binadamu za Kimarekani,” alisema Moaf.
Aliongeza kuwa iwapo Waislamu watauthamini vyema umuhimu wa Hija, basi ibada hiyo inaweza kuwa fursa ya kipekee ya kutekeleza Bara’at min al-Mushrikeen (kujikana kwa wazi washirikina na madhalimu).
Ayatollah Ruhollah Moussavi Khomeini, anayefahamika zaidi kama Imam Khomeini, ndiye aliyesimamia Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979 yaliyomuondoa Shah wa Iran aliyekuwa akiungwa mkono na Marekani.
Alizaliwa mwaka 1902, na alikua kuwa kiongozi mashuhuri wa mapambano ya taifa la Iran dhidi ya mfumo wa kifalme wa kiimla uliodumu kwa karne nyingi.
Imam Khomeini alifariki dunia na kurejea kwa Mola wake tarehe 3 Juni, 1989 akiwa na umri wa miaka 87.
3493294