IQNA

Msomi wa Bahrain

Hija ni wajibu wa kidini na kisiasa katika fikra za Imam Khomeini

21:41 - June 04, 2025
Habari ID: 3480789
IQNA – Kwa mujibu wa mtazamo wa Imam Khomeini (RA), Hija ni ibada isiyotenganishwa na wajibu wa kisiasa na wa kidini, amesema mwanazuoni mmoja kutoka Bahrain.

Sheikh Abdullah Daqqaq alitoa hotuba katika semina ya mtandaoni iliyopewa jina “Imamu Mkuu Khomeini (RA): Mfano wa Kuigwa wa Mabadiliko Katika Ulimwengu wa Kiislamu,” iliyoandaliwa Jumanne, Juni 3, na Shirika la Kimataifa la Habari za Qur’ani (IQNA).

Katika hotuba yake, alizungumzia mada “Hija na Maendeleo ya Harakati ya Kiitikadi ya Waislamu Katika Fikra za Imam Khomeini (RA).”

Sheikh Daqqaq alirejelea aya ya 3 ya Surah At-Tawbah isemayo:
Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina..."Akasema kuwa kwa mujibu wa fikra za Imam Khomeini, Hija haina maana bila ya Bara’at min al-mushrikiin – yaani kujitenga wazi na washirikina.

Akaeleza kuwa kuna tamko chanya na tamko hasi katika dhana hiyo.
“Unaposema ‘La ilaha illa Allah’, huu ni mtazamo hasi unaokanusha uungu kwa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Wakati huo huo, kuna tamko chanya, ambalo ni kusadiki uwepo wa Mungu mmoja wa kweli. Hija nayo ni tamko chanya, ni utiifu kwa Mungu mmoja. Kutufu kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na kumuabudu Yeye peke yake, hiyo ni kauli ya chanya. Lakini pia kuna upande wa kukana,  wa kujitenga na ushirikina na washirikina.”

Alisisitiza kuwa Hija ndiyo ishara yenye nguvu zaidi ya umoja miongoni mwa Waislamu.
“Inadhihirisha heshima, mshikamano na nguvu ya Waislamu mbele ya ubeberu wa dunia. Na hii ni kwa sababu tangazo la kujitenga na washirikina ni jambo la lazima.”

Sheikh Daqqaq aliendelea kusema kuwa Hija ina siri nyingi na malengo mengi, yote yakimfundisha mwanadamu kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Semina hii ya mtandaoni iliandaliwa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 36 tangu kufariki kwa muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Ruhullah Khomeini.

4285958

Kishikizo: imam khomeini hija
captcha