IQNA

Harakati ya Imam Hussein (AS) Katika Qur’ani Tukufu

15:59 - July 09, 2024
Habari ID: 3479093
IQNA - Katika baadhi ya aya za Qur'ani Tukufu kuna maelezo ambayo yanaweza kuwa yana yanaashiria shakhsia na harakati ya Imam Hussein (AS) au angalau shakhsia yake inaweza kuwa kielelezo wazi cha waymini.

Mauaji aliyofanyiwa Imam Husein (AS) na Yazid yalikuwa ni tukio kubwa na la kutisha kiasi kwamba lilirekodiwa katika historia.
 Imam Hussein (AS), ambaye ndiye aliyeunda hamasa hii, ni mhusika ambaye alizaliwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na alilelewa na Mtume (SAW) na Imam Ali (AS). Katika utotoni, alikuwepo wakati wa kuteremshwa kwa baadhi ya aya za Quran.

Qura'ni Tukufu ina baadhi ya aya ambamo ndani yake kuna maelezo ambayo yanaweza kuashiria shakhsia au harakati ya Imam Hussein (AS).

Imam Hussein (AS) alikuwa ni mjukuu wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na mmoja wa watu waliotajwa katika Aya ya Mawadda ambamo Mtume (sSAW) ameamrishwa kusema: “Siwaombi malipo isipokuwa kuwapenda jamaa zangu wa karibu." (Aya ya 23 ya Surat Ash-Shura)

 Wanachuoni wakubwa wa Hadithi kama Ahmad bin Hanbal, Ibn Munzar, Ibn Abi Hatam, Tabaraniy na Ibn Marduya wamemtaja Ibn Abbas akisema kuwa zilipoteremshwa aya hizi, Maswahaba walimuuliza Mtume (SAW) ni nani hao watu wanaotajwa katika aya hii  na  akajibu: Ali (AS) na Zahra (SA) na watoto wao wawili, Hassan (AS) na Hussein (AS).

Aya nyingine ni Ayat Tathir (Aya ya utakaso): “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara.". (Aya ya 33 ya Surah Al-Ahzab)

Kwa mujibu wa Hadith, "Watu wa Nyumba" inahusu Ali (AS), Zahra (SA), Hassan (AS) na Hussein (AS). Kwa mfano, imepokewa kutoka kwa Ummu Salama kwamba Mtume (SAW) alimwambia Hadhrat Zahra (AS) amlete mumewe na watoto. Walipokusanyika wote, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawafunika kwa Kisa (nguo) kisha akasoma Aya ya Tathir (Aya ya Ahl-ul-Bayt).

Marejeleo ya Qur'ani Kuhusu Mambo ya Maasi ya Imam Hussein
Aya ya Al-Mubahala ni aya nyingine ndani ya Quran ambamo ndani yake kuna rejea ya Imam Hussein (AS).

Tukio la Mubahila lilitokea katika mwaka wa 10 Hijiriya ambapo kundi la Wakristo, likiongozwa na Askofu wa Najran aitwaye Abdul Masih (au Abu Harisa), waliamua kujadiliana na Mtume (saw na kizazi chake) kuhusu asili ya Nabii Isa (amani iwe juu yake).

Ilikuja baada ya wao kupokea barua kutoka kwa Mtukufu Mtume (SAW) ikiwaita wawe Waislamu, na kukutana na kujadiliana baina yao wenyewe kuhusu yaliyomo ndani ya barua hiyo na majibu yanayofaa. 

Siku waliyoafikiana hapo awali, walikataa kufanya Mubahala kwa vile waliona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja na watu wa karibu wa familia yake, ambao ni binti yake, Fatima al-Zahra (SA), mkwe wake. , Imam Ali (AS), wajukuu zake, Hassan (AS) na Hussein (AS), na hivyo Wakristo walielewa ukweli wake. Kwa njia hii Mtume (SAW) alishinda katika tukio hili.

Katika Aya ya 61 ya Surat Al Imran inasema; “Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.”

Kwa mujibu wa Hadithi nyingi za Shia na Sunni, Mtume (SAW) alichukua pamoja naye tu Ali (AS), Zahra (SA), Hassan (AS) na Hussein (AS). Kwa hiyo “wana wetu” katika aya hii inawahusu Hassan (AS) na Hussein (AS).

3489036

captcha