
Imam Husein (AS) pamoja na masahaba zake walipigana na kuuawa kishahidi kwa ajili ya kutetea utu na heshima ya binadamu kwa namna ambayo yeyote atakayejifunza kuhusu tukio hilo katika historia atashuhudia kwamba Imam Hussein (AS) na masahaba wake walidhulumiwa.
Wapenda uhuru wengi duniani ambao wamepigania uhuru wa nchi zao na kukombolewa watu wao kutoka katika dhulma na utumwa wameipongeza harakati ya Imam Hussein (AS) na kuichukulia kuwa ni mfano wa kuigwa.
Mmoja maarufu ni Mahatma Gandhi, kiongozi wa kisiasa na kiroho wa Wahindu wa India ambaye aliongoza taifa lake kwenye njia ya ukombozi kutoka kwa ukoloni wa Uingereza alisema; “Nimesoma maisha ya Imamu Husein (AS), shahidi wa Uislamu, kwa makini na kwa umakini wa kutosha kwenye kurasa za Karbala, na ni wazi kwangu kwamba kama India inataka kuwa nchi yenye ushindi, inapaswa kufuata mfano wa Imam Hussein (AS).”
Zaidi ya hayo, utafiti wa ngano ya maisha ya Imam Hussein (AS) na harakati yake ya kihistoria umetia ilhamu na kuamsha moyo wa kila mwanafikra aliyepata kumfahamu mhusika huyo.
Edward Gibbon, mwandishi wa kitabu cha "Historia ya Kupungua na Kuanguka kwa Dola ya Kirumi", anaandika: "Katika karne zote zijazo, kusimulia na kuelezea tukio la kusikitisha na huzuni la kifo cha Imam Hussein (AS) kutasababisha ufahamu na usikivu wa mioyo. na nafsi kwa ajili ya wanadamu wote popote pale wawezapo kuwa.”
Mwanafikra, mwanafalsafa na mshairi wa Kipakistani Muhammad Iqbal (Lahori) aliandika kwamba Somo bora ambalo mtu anaweza kujifunza kutokana na mauaji ya Imamu Hussein ibn Ali (AS) ni kutafuta uhuru wa kiroho,na masahaba wake wa kweli wa Imam Hussein (AS) wanaweza tu kuwa wale ambao kwanza wanatafuta uhuru na kisha kuwasaidia wengine kuupata baada ya kuupata uhuru huo.
Harakati ya Imam Hussein (AS) Katika Qur’ani Tukufu
Zaidi ya hayo, tukio la Karbala hugusa hisia na kuleta machozi machoni kwa mtu.
Mtaalamu wa mambo ya Mashariki na mtafiti katika mafumbo ya Kiislamu Profesa Edward Browne alisema kuhusu hisia hizi safi: Je, hii inawezekana kwamba kunaweza kuwa na watu wachache ambao wanasikia hadithi ya Karbala lakini hawakasiriki na kuhuzunika? Hata wasio Waislamu hawawezi kukataa usafi wa kiroho ambao vita vya Kiislamu vilipiganwa chini yake.
Mambo mengi yamesemwa kuhusu sura hii kubwa ya historia ya Kiislamu.
Lakini juu ya yote, ukweli kwamba Imam Hussein (AS) ni mhusika ambaye hadithi yake ya maisha, kabla na wakati wa mauaji kwake, inatufundisha somo la kusimama imara katika njia ya ukweli.