IQNA

Dini

Mazungumzo ya Dini Mbalimbali ni Muhimu Ili Kupambana na chuki dhidi ya Uislamu

14:18 - July 30, 2024
Habari ID: 3479200
IQNA – Mwingiliano kati ya Waislamu na jumuiya nyingine ni muhimu kwa ajili ya kukuza maelewano na kuzuia kutokuelewana kunakochangia chuki dhidi ya Uislamu, amesema Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim.

Anwar alisema kuwa nchi za Magharibi, hata kipindi cha baada ya ukoloni, bado zinashikilia kanuni za zamani za kuibua mifarakani, kueneza habari potofu na chuki dhidi ya Uislamu.
"Unawezaje kuishi katika jamii kama Malaysia yenye watu wa makabila mbalimbali, ya dini nyingi na kuepuka kuwa na mazungumzo ya maelewano na dini, tamaduni, staarabu ... na kisha kudai Magharibi lazima watuelewe?
"Kwa hivyo nadhani kuna haja kuwafanya wengine watuelewe, na sisi kuwaelewa," alisema katika hotuba yake katika Mkutano wa 7 wa Dunia wa Mawazo na Ustaarabu wa Kiislamu (WCIT) 'Pamoja Tunasimama. : Waislamu na Ubinadamu Ulimwenguni'.
Waziri Mkuu pia aliwataka Waislamu kuelewa dhana ya kubadilishana maarifa na masomo.
“Mnatamani kupata yaliyo bora zaidi ya kuelewa na kufahamu, kama vile tulivyoelewa amri ya Qur’an, kwa kutumia maneno yanayofaa sana, sio tu kustahamiliana, bali lita’arafu yaani kufahamiana. Ni kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kuelewana, kufahamu tofauti.

3489277

Habari zinazohusiana
Kishikizo: malaysia dini
captcha