IQNA

Tamasha la Kiislamu

Tangazo kuhusu Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Qur'ani la Restu

21:29 - January 10, 2023
Habari ID: 3476383
TEHRAN (IQNA) – Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Qur'ani la Restu linatarajiwa kufanyika kuanzia Januari 20 hadi 29 huko Putrajaya, Malaysia, na waandaaji wametoa maelezo yake.

Hafla hiyo imeandaliwa na taasisi nyingi za Malaysia ikiwa ni pamoja na Wakfu wa Restu na washirika wa kigeni kama vile kituo cha kitamaduni cha Iran huko Malaysia na itafanyika katika Nasyrul Quran Complex huko Putrajaya.

Kulingana na kitabu cha programu kilichotolewa na waandaaji, hafla hiyo inawaruhusu wageni kushuhudia maonyesho maalum, na kuingiliana na wajasiriamali katika sekta za Qur'ani Tukufu na sanaa ya Kiislamu na bidhaa za Kiislamu huku pia wakijaribu kuboresha taswira ya Uislamu kama dini iliyojumuisha na ya amani.

Kuanzisha uhifadhi na ustawi wa Qur'ani Tukufu, kutukuza mafundisho ya Uislamu, kualika umma kupenda elimu na wanazuoni, kutumia teknolojia ya kisasa kama njia ya kuhubiri yenye ufanisi, na kujaribu kurudisha umma wa Kiislamu kwenye utambulisho wao wa kweli yametajwa miongoni mwa malengo mengine ya tamasha hilo.

3482023

captcha