IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 62 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia Yafunguliwa Rasmi + Video

11:54 - October 20, 2022
Habari ID: 3475957
TEHRAN (IQNA) –Mashindano ya 62 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Malaysia yalianza rasmi Jumatano usiku katika mji mkuu wa Malaysia wa Kuala Lumpur.

Sherehe ya ufunguzi ilihudhuriwa na washindani wa wanaume na wanawake, maafisa wa Malaysia, mabalozi wa  baadhi ya nchi za Kiislamu, na mamia ya watu wa Malaysia katika Kituo cha Mikutano cha Kuala Lumpur (KLCC).

Kwa mujibu wa droo hiyo, mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Masoud Nouri alikuwa mshiriki wa kwanza kufanya kisomo chake.

 

Huu hapa ni usomaji wa Nouri wa Surah Al-Imran, aya 156-164:

 

Kila mshiriki ana kati ya dakika 10 hadi 14 kubainsha uwezo wake.

Jopo la majaji linalojumuisha wataalamu kutoka nchi nane zikiwemo Malaysia, Misri, Jordan, Moroko na Indonesia

Moja ya sifa za mashindano ya mwaka huu ni kwamba waandaaji wanatumia teknolojia za kisasa kutoa tarjuma na tafsiri ya aya zinazosomwa  kwa hadhira kwenye ukumbi.

Mashindano hayo maarufu ya Qur'ani ya kimataifa yanatarajiwa kukamilika Oktoba 25 wakati washindi wakuu watakapotangazwa.

Mashindano ya 62 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Malaysia yalifanyika mtandaoni katika hatua ya awali ya mchujo. Mashindano hayo mwaka huu yanafanyika ana kwa ana katika ukumbi baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na janga la COVID-19.

Kulingana na maafisa, washiriki 41 kutoka nchi 31 wamepangwa kushiriki katika duru ya mwisho katika makundi mawili ya wanaume na wanawake.

Kuala Lumpur iliandaa toleo la 61 mwezi Aprili 2019 na mwakilishi wa Iran Hadi Movahed Amin alishika nafasi ya nne baada ya washiriki kutoka Malaysia, Algeria, na Moroko. Zaidi ya qari 100 na wahifadhi kutoka nchi 71 walishiriki katika toleo lililopita.

4093098

captcha