Toleo la 44 la Mashindano ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma na Kufasiri Qur'ani Tukufu yalianza katika mji huo mtukufu kwa awamu ya awali ya mchujo siku ya Ijumaa.
Siku ya Jumatatu Mohammad Hossein Behzadfar ambaye anaiwakilisha Iran katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu alipanda jukwaani kujibu maswali ya jopo la majaji katika duru ya awali.
Aliombwa asome aya za Qur'ani katika Sura Al-Nisa, At-Tawbah, Nahl, Ash-Shuara, na Al-Hadid.
Alijibu maswali yote bila matatizo yoyote na hakufanya makosa katika kusoma aya. Kwa mujibu wa tathimini, Ustadh Behzadfar anatarajiwa kutinga raundi ya mwisho kwa urahisi.
Mohammad Mehdi Rezaei ni mwakilishi mwingine wa Iran ambaye anashindana katika kitengo cha kuhifadhi Juzuu 15 za Qur'ani.
Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, imeandaa mashindano hayo katika Msikiti Mkuu wa Makka kati ya Safar 5 na 17, 1446 AH (Agosti 9 na 21, 2024).
Kuna jumla ya washiriki 174 kutoka nchi 123 wanaoshiriki katika hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani.
3489493