IQNA

16:29 - January 20, 2021
News ID: 3473576
TEHRAN (IQNA) – Semi fainali ya kusoma Qur'ani Tukufu au qiraa katika Awamu ya 37 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran imemalizika leo Jumatano.

Washiriki walikuwa ni kutoka Bangladesh, Thailand, Chad, Iraq, Cameroon, Lebanon, Mauritania, Nigeria, Misri, na Uholanizi pamoja na nchi zingine kadhaa.

Kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu imeanza leo alasiri na itaendelea hadi Alhamisi Alasiri. Majaji katika mashindano hayo ni kutoka Iran, Syria, Sudan, Iraq, Lebanon na Indonesia.

Mashindano hayo ya nusu fainali yanafanyika kwa njia ya intaneti kutokana na janga la COVID-19 au corona.

Mehdi Qarasheikhlu, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu na Misaada la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mahojiano na IQNA, amesema semi fainali ya mashindano hayo inajumuisha washiriki 120 kutoka nchi 70. Washiriki takribani 50 wanatazamiwa kufika fainali ya mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Aidha amesema katika duru za awali kulikuwa na washiriki 600 kutoka nchi 70. Ameongeza kuwa, mashindano hayo ya semi fainali ambayo yanafanyika kwa njia ya intaneti yataendelea hadi Januari 21.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Kutokana na janga la COVID-19 mashindano hayo hayakufanyika mwaka 2020 na yalifanyika mara ya mwish Aprili 2019 mjini Tehran ambapo kulikuwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 36.

3948862

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: