IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Umoja wa Kiislamu wadhihirika katika Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran

20:21 - September 20, 2022
Habari ID: 3475813
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Wakfu na Misaada la Iran ameeleza kushiriki kwa wananchi wa madhehebu ya Shia na Sunni kwa pamoja katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni dhihirisho la umoja wa Kiislamu nchini.

Hamid Majidimehr ameliambia  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) kwamba Waislamu wa madhehebu ya Sunni walishiriki kwa wingi katika duru ya majimbo ya Mashindano ya 45 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran, hususan katika majimbo kama Kurdistan, Sistan na Baluchestan, Hormozgan, Azarbaijan Magharibi, Bushehr, Khorasan Kusini na Golestan.

Vile vile amebainisha kuwa wananchi wanaofuata madhehebu ya Sunni nchini Iran  walishiriki kwa wingi katika kategoria ya tafsiri ya Qur'ani kwa kuzingatia vyanzo vya Tafsir vya Kisunni.

Pia, wataalamu wa Qur'ani kutoka miongoni wasomi wa Kisunni walialikwa kuhudumu kama wajumbe wa jopo la majaji katika mashindano hayo, afisa huyo alibainisha.

Haya yote ni maonyesho ya umoja na ukaribu wa madhehebu za Kiislamu zenye msingi wa Qur'ani Tukufu, aliongeza.

Kulingana na afisa huyo, jumla ya Wasunni 1,853 kutoka mikoa 27 walihudhuria kiwango cha mkoa cha mashindano hayo.

Majidimehr pia alibainisha kuwa watu wa dini kutoka imani nyingine kama Ukristo na Uzarathustra (Zoroastrianism) pia wamealikwa katika mashindano hayo ya kitaifa ya Qur'ani.

Duru ya mwisho inapangwa kufanyika katika jimbo la kusini-magharibi la Khuzestan katika mwezi wa Dey (Desemba 2022-Januari 2023).

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Shirika la Wakfu na Misaada la Iran  kwa kushirikisha wanaharakati wakuu wa Qur'ani kutoka kote nchini.

Manifestation of Unity at Iran Nat’l Quran Contest

Manifestation of Unity at Iran Nat’l Quran Contest

4086435

Kishikizo: mashindano ya qurani ، iran
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha