IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yamepangwa nchini Kuwait mwezi Oktoba

16:09 - August 15, 2022
Habari ID: 3475624
TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Kuwait yataandaliwa tena mwaka huu baada ya kusitishwa kwa muda wa miaka mitatu.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo ya Kiarabu imesema duru ya 11 Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani itafanyika mwezi Oktoba chini ya usimamizi wa Amir wa Kuwait Sheikh Nawab Ahmed Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.

Wizara hiyo ilisema itaanza Oktoba 20 na wagombeaji watashindana katika kuhifadhi Qur'ani, usomaji na Tajweed, iliripoti Al-Watan.

Kustawisha uwezo wa kuhifadhi Qur'ani, kubainisha vipaji vya juu vya Qur'ani, na kuhimiza Umma wa Kiislamu na Kiarabu kujifunza sayansi ya qiraa (mitindo ya usomaji Qur'ani) ni miongoni mwa malengo ya shindano hilo.

Wizara hiyo iliendelea kusema kuwa kuandaa shindano hilo kunaashiria kuwa Kuwait ni nchi hai katika nyanja za Qur'ani.

Toleo la 10 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Kuwait, yanayojulikana kama Tuzo ya Qur'ani ya Kuwait, ilifanyika mwaka 2019,

Mohammad Yusuf Darvishi kutoka Mkoa wa Qazvin na Hamid Reza Moqaddadi kutoka Mkoa wa Razavi Khorasan waliiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kategoria zake mbili.

Mnamo 2020 na 2021, Kuwait ilisitisha hafla ya Kurani kwa sababu ya janga la corona.

Kuwait ni nchi ya Kiarabu yenye Waislamu wengi katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

3480102

captcha