IQNA

Muqawama

Sheikh Naim Qassim: Mustakabali wa eneo utainishwa na Mapambano ya Kiislamu (Muqawama)

10:53 - October 31, 2024
Habari ID: 3479674
IQNA - Katibu Mkuu mpya wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuendelea kwa mapambano ya kuvuruga njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo zima la Asia Magharibu na kusema kuwa Mapambano ya Kiislamu (muqawama) Gaza na Lebanon ni kielelezo cha adhama ambacho kitajenga mustakbali wa eneo hilo.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa njia ya televisheni kama Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama nchini Lebanon siku ya Jumatano, Sheikh Naim Qassem alionya kwamba utawala wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi na Ulaya wanashiriki katika "mpango mkubwa" wa kutawala eneo la Asia Magharibi.
Aliwaambia hadhira kwamba, mpango wake wa kivitendo ni kuendeleza njia na kazi ya mtangulizi wake, Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah. Sheikh Qassem amebainisha kuwa, "Tutaendelea kutekeleza mpango wa vita uliowekwa na Sayyid Nasrullah, na tutabaki kwenye njia ya vita ndani ya mwelekeo wa kisiasa uliowekwa."
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, kuiunga mkono Gaza ni muhimu ili kukabiliana na hatari inayoletwa na utawala wa Kizayuni kwa eneo zima.
Kadhalika Sheikh Qassem amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel haujawahi kufuata sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
"Israel haijawahi kufungamana na Azimio Nambari 1701, na imekiuka mamlaka ya anga na bahari ya Lebanon mara 39,000," alisema, akiashiria azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililomaliza vita vya 2006, na kutaka kuheshimiwa uhuru na mamlaka ya kuhjitawala Lebanon
Kiongozi huyo wa Hizbullah ameeleza bayana kuwa, ni Muqawama na wala sio maazimio ya kimataifa, ambao ulivifurusha vikosi vya Israeli kutoka Lebanon mwaka 2000.
 3490501

captcha