Sheikh Qassem amesisitiza kuwa aidiolojia ya Israel, vitendo vyake na hujuma zake ni hatari kwa Waislamu, Wakristo na Wayahudi na zinayumbisha amani ya kikanda na kimataifa.
Kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon amesema: Tangu kuanza kutekelezwa mapatano ya kusimamisha vita kati ya Lebanon na Israel; utawala huo haujasitisha mashambulizi na jinai zake na umekiuka mapoatano hayo zaidi ya mara 3,700.
Amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni unapasa kuheshimu masharti uliyokubaliana na Lebanon na kuacha vitendo vyake vya uchokozi.
Sheikh Qassem amesema Hizbullah haitayumbishwa na vitisho, wala haitakubali kusalimisha silaha zake kwa Israel. "Hatutakubali kudhalilishwa, kuacha ardhi yetu au kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni mkabala wa vitisho," ameeleza Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon.
Ameongeza kuwa: Mapambano yanayoendeshwa na harakati ya Hizbullah ni ulinzi dhidi ya tishio la kimkakati linaloyakabili mataifa mengi, ikiwa ni pamoja na Palestina, Lebanon, Misri, Syria na Jordan.
4292309