IQNA

Rambirambi

‘Kifo cha kishahidi cha Nasrallah Kimefungua Sura Mpya katika Vita dhidi ya Utawala wa Kizayuni’

21:38 - September 29, 2024
Habari ID: 3479509
IQNA – Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran, amelaani vikali mauaji ya kigaidi yaliyotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi Sayed Hassan Nasrallah na kusisitiza kwamba kuuawa shahidi kiongozi wa Hizbullah kutafungua ukurasa mpya katika vita dhidi ya Israel.

Ifuatayao ni taarifa hiyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

“Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.” (Qur’ani Tukufu, Al Imran: 169)

Baada ya kufanya jinai mbaya zaidi dhidi ya watu wa Ghaza kwa muda wa mwaka mmoja, utawala ghasibu wa Israel kwa mara nyingine umefichua tabia yake ya kikatili na ya kigaidi kwa kumuua kiongozi wa muqawama, Haj Sayyed Hassan Nasrallah.

Bila shaka, kuuawa shahidi mwanajeshi huyo mashuhuri wa mapambano kutakuwa na nafasi muhimu katika kuenea kwa Jihad ya uhuru dhidi ya utawala ghasibu wa Israel unaoikalia kwa mabavu umwagaji damu, na hivyo kufungua sura mpya katika vita vya mapambano dhidi ya Uzayuni wenye misimamo mikali.

Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS anapenda kuchukua fursa hii kutoa salamu za rambirambi na pongezi kwa Imam Mahdi, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, maulama wakubwa, taifa la Lebanon, wapiganaji wa muqawama na Waislamu wote wanaotii amri ya Kiongozi Muadhamu kusimama bega kwa bega na mrengo wa muqawama, haswa na Hizbullah ya Lebanon. Tunatumai , kwa baraka za Imam Ridha, mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi ushindi na ukombozi wa Al-Quds.

Kama ilivyoelezwa na Kiongozi Muadhamu, ujumbe wa maisha yenye matunda ya Imam Ridha ulikuwa ni ‘Mapigano ya Kudumu na Bila Kuchoka’. Kwa hivyo, katika kipindi hiki cha kihistoria, Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS kwa unyenyekevu anawataka wapigania uhuru wote kutii mafundisho ya Kiislamu na kusimama kidete dhidi ya jinai zisizo na kikomo za utawala ghasibu wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi hususan Marekani.

Ahadi ya Mwenyezi Mungu bila shaka itatimia kwa muda mfupi, na vita hivi vitaisha kwa ushindi wa Mrengo wa Muqawama (Mapambano ya Kiislamu).

3490072

Habari zinazohusiana
captcha