IQNA

Diplomasia

Mkuu wa Al-Azhar apongeza misimamo ya Estonia katika kuunga mkono Palestina

21:18 - November 08, 2024
Habari ID: 3479719
IQNA – Shekhe mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri amepongeza misimamo ya Estonia dhidi ya utawala wa Israel.

Katika mkutano na Rais Alar Karis wa Estonia, Sheikh Ahmed al-Tayeb alipongeza hatua ya nchi hiyo kulaani uvamizi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kura yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuunga mkono uanachama wa Palestina.
Alisema misimamo hii inadhihirisha dhamira ya nchi hiyo ya kutetera kanuni za kibinadamu na haki ya kimataifa na kuongeza matumaini kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono haki halali za Wapalestina.
Akielezea mauaji ya watu wa Ukanda wa Gaza, Sheikh al-Tayeb alisema ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel haufikiriki na hauelezeki.
Alisema watu wa Gaza hawajafanya uhalifu wowote bali wamesisitiza tu kusalia katika ardhi yao na kukataa kuihama.
Kwingineko katika matamshi yake, Sheikh al-Tayeb alifafanua kuhusu shughuli za Al-Azhar, akisema mkabala wake kwa zaidi ya miaka elfu moja taasisi hiyo imekuwa ikihimiza ujumbe wa kueneza amani duniani.
Aliongeza kuwa Al-Azhar ina wanafunzi zaidi ya 60,000 kutoka zaidi ya nchi 100.
Alielezea utayari wa kituo hicho kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kiislamu wa Estonia wanaotaka kusoma Al-Azhar.

3490597

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al azhar gaza tayeb
captcha