IQNA

Uislamu Duniani

Waislamu wa Peru wapokea nakala za Qur'ani zenye tarjuma ya Kihispania

14:39 - November 16, 2024
Habari ID: 3479760
IQNA - Jumuiya ya Kiislamu ya Peru huko Lima imetunukiwa zawadi ya nakala 50 za Qur'ani Tukufu zenye tarjuma ya Kihispania.

Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim alikabidhi kituo hicho nakala hizo za Qur'ani katika ziara yake katika nchi hiyo ya Amerika Kusini siku ya Ijumaa.

Anwar Ibrahim na mkuu wa jumuiya hiyo, Murad Hamida, walifanya mkutano ambapo walijadili maendeleo ya jumuiya ya Waislamu nchini Peru.

Pia walizungumza kuhusu kujitolea kwa Malaysia kuwezesha michakato ya uidhinishaji wa bidhaa na huduma Halal na kusaidia katika elimu ya Kiislamu na Da’wah miongoni mwa jamii ya Waislamu nchini Peru.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Malaysia nchini Peru, ambayo inajumuisha ushiriki wake katika Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Kiuchumi wa APEC (AELM) inatarajiwa kuimarisha uhusiano wa nchi mbili kati ya Kuala Lumpur na Lima.

Peru, ni nchi ya Amerika Kusini inayopakana na Ecuador, Colombia na Brazil. Peru inakadiriwa kuwa na idadi ya watu karibu milioni 34, na karibu Waislamu 10,000.

Jumuiya ya Waislamu nchini Peru kwa kiasi kikubwa inajumuisha wahamiaji kutoka nchi kama vile Lebanon na Palestina, na pia kuna idadi ndogo ya Waperu asilia ambao wamesilimu.

3490697

captcha