"Lengo letu kuu ni kuunda uelewa sahihi wa Qur’ani," Khamoushi alisema wakati wa kuhutubia sherehe ya kufunga sehemu ya maarifa ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur’ani ya Iran huko Qom Alhamisi. Akiashiria aya ya Qur’ani inayoashiria lengo hili isemayo, " Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni." (Surah An-Nur, aya ya 36), Khamoushi alisisitiza kwamba uelewa wa Qur’ani unapaswa kuwa kipaumbele kwa watu binafsi, familia, jamii, na mifumo ya kisiasa.
Alisisitiza pia jukumu la mashindano ya Qur’ani katika kutathmini ukuaji wa uelewa wa Quran ndani ya jamii. "Mashindano haya ni kisingizio cha kuona jinsi uelewa wa Quran umekua katika jamii," alisema. Akigusia changamoto zilizowekwa na vikundi vya misimamo mikali duniani, Khamoushi alisema kwamba makundi kama Daesh yaliundwa ili kuzuia kuenea kwa mawazo sahihi ya Kiislamu. "Waliunda Daesh ili kuzuia kuenea kwa mawazo safi ya Kiislamu duniani na kuwaonyesha Waislamu kama watu wasio na huruma wanaowakata wengine vichwa wakiwa wanasema 'Allahu Akbar'. Hii ilikuwa kuzuia kuenea kwa uelewa sahihi wa Qur’ani duniani," alibaini. Khamoushi alisema kuna changamoto katika kutekeleza mafundisho ya Qur’an katika maisha ya kila siku na huku akisisitiza umuhimu wa elimu endelevu na kamili ya Qur’ani alisema: "Tunataka kuwalea watoto wetu kwa mtazamo wa kidunia, lakini tunapaswa kuelewa kwamba hii ni makosa. Uislamu sio kwa ajili ya malezi ya kidunia pekee; toleo lake kamili ni kwa ajili ya dunia na akhera kwani baada ya maisha ya duniani hatimaye turarejea kwa Mola Muumba. Amesema elimu endelevu na kamili ya Qur’ani Tukufu lazima iwe lengo la malezi, huku akifafanua nukta hiyo kwa aya ya Qur’ani ifuatayo: "Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto..."Sehemu ya aya ya 20 ya Surah Al Hadid ya Qur'ani Tukufu
Alisisitiza dhamira ya shirika lake ya kukuza maisha ya Qur’ani na kusema. "Mashindano ya Quran yamekuwa na yataendelea kufanyika, lakini lengo letu kuu ni kubadilisha mtindo wa maisha uwe ni wa Qur’ani kikamilifu sambamba na kueneza uelewa sahihi wa Quran." Sherehe hiyo iliashiria mwisho wa Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur’ani ya Iran. Sehemu za usomaji na kuhifadhi za mashindano zilifanyika mapema mwezi huu huko Tabriz, Mkoa wa Azarbaijan Mashariki.
3491224