Abu Sneineh aliwaambia waandishi wa habari kwamba askari wa jeshi ghasibu la Israel walimsimamisha kwenye lango la ukaguzi alipokuwa akielekea eneo lake la kazi katika msikiti huo siku ya Jumanne na kutaka kitambulisho chake na kumwamuru avue nguo zake ili aweze kukaguliwa.
Aliongeza kuwa alikataa kupekuliwa hadharani, hivyo askari watano walimpeleka kwenye chumba kilichofungwa na kumpiga vikali na kumtusi.
Abu Sneineh alieleza kuwa askari walimruhusu kuingia msikitini baada ya kupigwa, lakini waliwazuia wafanyakazi wa gari la wagonjwa kuingia eneo hilo ili kumpatia matibabu.
Aliongeza kuwa shambulio hilo halijawahi kutokea, akibainisha kuwa "amekuwa akifanya kazi msikitini kwa zaidi ya miaka kumi na anaingia kila siku, na askari wanamfahamu vyema.
Abu Sneineh alisema vikosi vya utawala ghasibu wa Israel vimezidisha ukiukaji wao dhidi ya msikiti na waumini tangu tarehe 7 Oktoba 2023, na kufunga milango yote ya msikiti isipokuwa moja, huku kukiwa na ulinzi mkali na misako ya kila siku na ya kudhalilisha waumini wa Kiislamu.
"Mwaka huu, utawala wa Israel ulifunga Msikiti wa Ibrahimi kwa siku 13 kwa waumini wa Kiislamu, huku ukifunguliwa kabisa kwa walowezi, kinyume na Mkataba wa Hebroni
3491283.