Katika ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya X, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alipongeza uteuzi huo.
Alisema anafurahi kwamba pengo lililopatikana baada ya kuuawa shahidi Sayed Hassan Nasrallah imejazwa baada ya kuchaguliwa kwa Sheikh Qassem.
Sheikh Al Khalili amesema mkuu huyo mpya wa Hizbullah ataendeleza njia ya shahidi Nasrallah katika kukabiliana na hujuma za kikatili za utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon na mataifa mengine ya kieneo.
Vile vile alitumai kuwa Sheikh Qassem atatekeleza jukumu hilo kwa uthabiti, ushujaa na subira hadi ushindi wa mwisho na ukombozi wa ardhi za Waislamu kutoka kwa utawala ghasibu wa Israel.
Wiki iliyopita, Sheikh Qassem, ambaye alihudumu kama naibu mkuu wa Hizbullah tangu 1991, alichukua nafasi ya Shahidi Nasrallah, ambaye aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la utawala haramu wa Israel kwenye kitongoji cha Beirut mnamo Septemba 27.
Sheikh Qassem alikuwa miongoni mwa watu waliochangia kuanzishwa kwa Hizbullah na harakati ya Amal.
4246173