Baada ya Asma Falaki, qari wa heshima, kusoma aya kutoka katika Qur’ani Tukufu, washiriki walianza kupanda jukwaani kulingana na ratiba yao.
Washiriki katika kitengo cha wanawake siku ya kwanza ya fainali walikuwa:
Zaynab Abdul Rahman kutoka Ghana (mhifadhi Qur’ani yote),
Masoumeh Mohammadi kutoka Afghanistan (Tarteel),
Ifnan Rashad Ali Yaqub kutoka Yemen (amehifadhi),
Jamliaya Abdulqadir kutoka Ufilipino (Tarteel),
Hana Ali Mirafi kutoka Nigeria (amehifadhi),
Hura Haydar Hamzi kutoka Lebanon (Tarteel), na
Karima Haj Brahim kutoka Thailand (Tarteel).
Kipindi cha asubuhi kilihitimishwa kwa usomaji wa Quran na qari mwingine wa heshima, Marziyeh Mirzaeipour.
Mashindano katika kitengo cha wanaume yanafanyika katika vipindi vya alasiri.
Wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani Tukufu kutoka nchi 144 walishiriki katika hatua za awali za mashindano haya, na kutoka kwao, wawakilishi kutoka nchi 27 wamefanikiwa kufika katika hatua ya fainali kwenye vipengele vya wanaume na wanawake.
Fainali hizi, zinazofanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran, zitafikia tamati katika hafla ya kufunga ambapo washindi wa juu watatangazwa na kutunukiwa tuzo.
Mashindano ya Kimataifa ya Qu’rani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Awqaf na Masuala ya Hisani la nchi hiyo.
Lengo lake ni kukuza utamaduni na maadili ya Qur’ani Tukufu miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qu’rani.