IQNA

Waislamu watakiwa wasusie tende za 'Israel' zijulikanazo kama MyJool

17:37 - February 26, 2025
Habari ID: 3480272
IQNA – Huku mwezi mtukufu wa Ramadhani ukikaribia, kumekithiri kampeni za kususia tende zinazozalishwa au kufungashwa katika maeneo ya Palestina ambayo yametekwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa Kampeni ya Mshikamano na Palestina, tende zinazozalishwa katika vitongoji haramu katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu aghalabu zinauzwa kwa jina la tende za MyJool au Medjool.

Inasema kwenye tovuti yake, “Kila wakati angalia lebo wakati wa kununua tende. Usinunue tende zinazozalishwa au kufungashwa katika maeneo yanayokaliwa au makazi ya Ukingo wa Magharibi. Ikiwa hakuna jina la nchi  kwenye boksi, angalia tovuti ya muuzaji.”

Kampeni hiyo inatoa wito kwa Waislamu wote kutofuturu kwa tende za Israel katika mwezi wa Ramadhani. “Simama kwa mshikamano na watu wa Palestina.”

Kulingana na kundi la Friends of Al-Aqsa au Marafiki wa Al Aqsa (FOA) lenye makao yake London, Palestina inayokaliwa kimabavu ni mzalishaji mkubwa zaidi wa tende za MyJool duniani.

Ilisema kuwa asilimia kubwa ya tende hizi zinasafirishwa Ulaya na kuuzwa katika maduka makubwa na madogo.

FOA ilisema katika ripoti kwamba sehemu kubwa ya tende za MyJool zinazoingizwa na Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Hispania na Italia.

Mnamo mwaka 2020, Uingereza iliingiza zaidi ya tani 3,000 za tende zenye thamani ya pauni milioni 7.5 ($8.9 milioni).

Inakadiriwa kuwa Israel inazalisha takriban tani 100,000 za tende kila mwaka.

Utawala wa Israel hupata karibu dola milioni 100 kutokana na kuuza nje tende kila mwaka, nyingi ambazo zinauzwa katika Ramadhani.

3492043

Kishikizo: tende israel ramadhani
captcha