IQNA

Kususia utawala bandia wa Israel

Waungaji mkono Palestina wazindua kampeni ya kususia bidhaa za Israeli Mwezi wa Ramadhani nchini Uingereza

22:51 - March 18, 2023
Habari ID: 3476724
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya vipeperushi 20,000 vinavyowahimiza Waislamu kutizama lebo yaani #CheckTheLabel na kususia bidhaa za utawala haramu wa Israel vimesambazwa katika misikiti kote Uingereza, sanjari na Ijumaa ya mwisho kabla ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, waandaaji walisema Ijumaa.

Mpango huo ni sehemu ya kampeni iliyoanzishwa na Jumuiya ya Marafiki wa Al-Aqsa (FOA) yenye makao yake nchini Uingereza - inayohusika na kutetea haki za binadamu za Wapalestina na kulinda Msikiti Mtakatifu wa Al-Aqsa huko  Al  Quds (Jerusalem)- ya "Kuangalia Lebo," na inatoa wito kwa Waislamu nchini Uingereza na duniani kwa ujumla kutofungua saumu zao kwa tendo zitokazo Israel ambazo zimetajwa kuwa “ladha ya ubaguzi wa rangi.”

Kampeni ya kususia imepata kasi kubwa katika kipindi cha kuelekea Mwezi Mtukufu Ramadhani mwaka huu, kupitia matangazo ya vyombo vya habari kutoka Uingereza hadi Morocco na Malaysia, FOA ilisema katika taarifa.

"Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2010, #CheckTheLabel imekuwa na athari isiyo na kifani kwa uelewa wa umma wa Uingereza juu ya uhusiano kati ya bidhaa wanazonunua na uvamizi haramu wa Israeli katika ardhi za Palestina  na sasa watu wengi wanazingatia maadili na huepuka kununua bidhaa za Israel kutokana na kampeni hii,” FOA ilisema.

"Ramadhan hii, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwamba tususie Israel," Shamiul Joarder, mkuu wa masuala ya umma katika FOA alisema. "Kwa kuangalia lebo na kuepuka tende za Israel, tunaweza kutuma ujumbe wazi: Hatutatoa pesa zetu kwa taifa la ubaguzi wa rangi ambalo linavunja sheria za kimataifa na kuua watoto wa Palestina."

Shirika hilo linasema kuwa Israel imewaua Wapalestina wasiopungua 83 katika siku 76 za kwanza za 2023, wakiwemo watoto wasiopungua 16.

"Miezi 3 ya kwanza ya 2023 imeshuhudia ghasia mbaya zaidi za Israeli dhidi ya Wapalestina katika miongo kadhaa na kuna wasiwasi juu ya mashambulio ya Israeli kwenye msikiti wa Al-Aqsa wakati wa Ramadhani," ilisema taarifa hiyo.

FOA imebaini kuwa "Israel ndio mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa tende aina ya Medjool, na asilimia 50 ya tende za Israeli zinauzwa Ulaya. "Tende hizi zinauzwa katika maduka makubwa makubwa pamoja na maduka madogo katika bara zima la Ulaya."

FOA inasema kuwa asilimia 50 ya tende za Israel zinasafirishwa kwenda Ulaya, ambapo Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Uhispania na Italia huagiza kiasi kikubwa cha tende hizo zilizokaushwa. Mnamo 2020 Uingereza iliagiza zaidi ya tani 3,000 za tende kutoka Israeli, zenye thamani ya takriban pauni milioni 7.5.

4128755

captcha