IQNA

Wapalestina katika Mwezi wa Ramadhani

Mhubiri wa Palestina: Waislamu wawaombee Wapalestina wa Gaza Mwezi wa Ramadhani

22:23 - March 12, 2024
Habari ID: 3478495
IQNA - Rais wa Jumuiya ya Wahubiri wa Kiislamu Palestina ametoa wito kwa Waislamu wote wanaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani waombe dua kwa ajili kukomeshwa mateso na masaibu wanayokumbana nao watu wa Gaza.

 

Sheikh Salman Abu Tariq al-Saudi aliyasema hayo katika ujumbe wa video kwa Shirika la Habari la IQNA kwa mnasaba wa kuanza kwa Ramadhani.

Waislamu wamuombea Mwenyezi Mungu, amalizie mateso na njaa kwa wananchi wa Ukanda wa Gaza ambao kwa hakika wamefunga kula kwa zaidi ya miezi mitano na kuwapa usalama, alisema.

Vile vile ameomba Mwenyezi Mungu aijaalie Ramadhani kuwa mwezi wa amani, usalama, ushindi na baraka kwa watu wa Palestina hususan Ukanda wa Gaza na Umma wote wa Kiislamu.

Alitumai kwamba, kwa neema za Mwenyezi Mungu, nyoyo za Waislamu zitakaribiana zaidi, tofauti zitaondolewa na umoja utatawala katika ulimwengu wa Kiislamu.

 Kwingineko katika ujumbe huo, al-Saudi aliomba kwamba Mwenyezi Mungu awaadhibu maadui wa Palestina na wahaini ambao wamekuwa wakiwasaidia.

Jumatatu iliadhimisha mwanzo wa Ramadhani, ambapo Waislamu hujinyima chakula na maji kuanzia mawio hadi machweo, huko Gaza, ambapo wakazi wote milioni 2.2 hawawezi kukidhi mahitaji yao ya chakula.

Israel ilianzisha vita vyake vya kuua Gaza mnamo Oktoba 7, 2023. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, wapalestina wasiopungua 31,045 wameuawa na 72,654 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israeli. Takriban asilimia 72 ya waathiriwa ni watoto na wanawake.

Zaidi ya miezi mitano ya mashambulizi ya kikatili ya Israel pia yamesababisha njaa kali miongoni mwa Wagaza.

Takriban watu 25, wengi wao wakiwa watoto, wamekufa kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini katika ardhi ya Palestina katika siku za hivi karibuni.

Utawala dhalimu wa Israel umezuia kuingia kwa chakula na vifaa vya msaada katika Gaza na kuondoa huduma zake za afya.

3487528

Habari zinazohusiana
captcha