IQNA

Maonyesho ya Nakala za Kale za Qur'ani Tukufu nchini Marekani+PICHA

15:53 - October 22, 2016
Habari ID: 3470626
Nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa mkono karne saba zilizopita zimeanza kuonyesha katika Taasisi ya Smithsonian, mjini Washington nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho ya nakala hizo za kale za Qura'ni ambazo ni za Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu huko Istanbul Uturuki, yameanza leo Jumamosi.

Nakala hizo za kale za Qur'ani zimetajwa kuwa muhimu kuwahi kuandikwa katika eneo la kijiografia kutoka Uturuki hadi Afghanistan kati ya karne ya 8 na 17 Miladia.

Mbali na maonyesho ya nakala hizo 18 za Qur'ani Tukufu, kutakuwa pia na warsha na vikao kuhusu Sanaa za Kiislamu, simulizi, kaligrafia na Sanaa za mkono. Aidha kutafanyika kongamano la Qur'ani Desemba Mosi katika Ubalozi wa Uturuki mjini Washington.

Maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Utamaduni ya Uturuki kwa ushirikiano na Jumba la Makumbusho la Smithsonian yamepewa anwani ya, "Sanaa ya Qur'ani: Johari Kutoka Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu na Uturuki' na yataendelea hadi Februari 20 mwakani.

3539488

Maonyesho ya Nakala za Kale za Qur'ani Tukufu nchini Marekani

captcha