IQNA

Bango la Siku ya Kimataifa ya Quds Lazinduliwa

13:06 - March 25, 2025
1
Habari ID: 3480437
IQNA – Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) imetayarisha bango la Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu wa 1446 H sawa na 2025.

Bango hilo limezinduliwa leo Jumatatu jijini Tehran katika kikao kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa WFPIST Hujjatul Islam Hamid Shahriyari na maafisa wengine kadhaa. 

Bango hilo lenye kauli mbiu ya “Ewe Al-Quds, Tunafungamana na Ahadi Yetu!” lina muundo wa Qubbat Sakhra katika Msikiti wa Al-Aqsa kama alama ya Al-Quds (Jerusalem), ambapo kuba lake limezungukwa na bendera za nchi za Kiislamu.

Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu itakuwa Ijumaa, Machi 28.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni miongoni mwa urithi wa mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Ammrehemu), ambaye anaheshimiwa kama kiongozi wa kiroho na Waislamu duniani kote. 

Poster of Int’l Quds Day Unveiled   

Mnamo mwaka 1979, muda mfupi baada ya kuongoza ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambayo yalimpindua mtawala wa kiimla, Shah, aliyeungwa mkono na Marekani pamoja na Israel, Imam Khomeini aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa Quds ili Waislamu na wapenda haki kote duniani waweze kujitokeza katika siku hiyo katika maandamano na mijumuiko ya kuunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina sambamba na kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikoloni na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Mji wa al-Quds (Jerusalem) unachukuliwa kuwa nembo ya ukombozi wa Palestina kwani unatazamiwa kuwa mji mkuu wa nchi huru ya Palestina.

 4273609

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
HASSAN ABDULLA KHAMIS
0
0
Ni jambo la wajibu kuwa na jukwa kama hili. Suala la ukombozi wa taiga la Palestina ni suala la utu na ubinadamu kanla ya kuwa la kiislamu.
Ni wajibu kila mtu kulisaidi kwa hali na Mali taiga joli lense kudhulumiwa asubuhi na jioni.

Siku ya Qudsi ni siku muhimi kwa umma wa kiislamu na kila mpenda haki uadilifu na unaware.
Tukumbuke madhila namatatizo ya maisha ya ndugu zetu wapalestina, na tusichoke kupaza Saudi zetu kwenye majukwaaa ya kimataifa tukidai haki za taifa hurt la palestina.

Tusichoke, bali tuendelee kuwa Bega kwa Bega na ndugu zetu tukimuweka mbele Allah katika kudai haki kamili za taiga hurt la Palestina.

Ahsante
captcha