IQNA

Qur'ani na Palestina

Wanafunzi Milioni 3 Iran wahudhuria vikao vya Qur'ani kwa ajili ya mashahidi wa Gaza

20:48 - April 09, 2024
Habari ID: 3478660
IQNA - Programu khitma ya Qur'ani zilifanyika Jumatatu katika shule zaidi ya 20,000 nchini Iran na nchi kadhaa duaniani kuwakumbuka mashahidi mabarobaro Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Mikaeil Baqeri, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Qur'ani, Etrat na Sala ya Wizara ya Elimu ya Iran, aliiambia IQNA kwamba wanafunzi milioni tatu wa shule nchini Iran walishiriki katika vikao hivyo vya Qur'ani ambavyo vilifanyika kuanzia saa tatu asubuhi Jumatatu ndani ya shule.

Kulikuwa na vikao vya khitma ya Qu'rani pia katika nchi kama vile India, Afghanistan, Pakistan, Senegal, Denmark na Sierra Leone, alisema.

Programu hizo zilijumuisha usomaji wa aya za Qur'ani Tukufu na ufafanuzi wa maana za aya hizo, Baqeri alisema.

Aidha amerejea Mpango wa Qur’ani “Kuishi na Aya”, uliofanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu nchini Iran na kusema kwamba, kama sehemu ya mpango huo, wanafunzi hao pia walisoma kwaya Aya ya 18 ya Sura Al-Hashr: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda."

Baqeri ametoa shukrani kwa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na kanali ya watoto ya Pouya TV kwa kuangazia ipasavyo matukio ya Qur'ani.

Tangu kuanza hujuma ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, zaidi ya Wapalestina 33,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuawa na utawala huo wa Kizayuni.

Miongoni mwa waliouawa shahidi huko Gaza katika kipindi cha miezi sita ya uvamizi wa Israel ni vijana wengi na wanafunzi wa shule.

4209345

Habari zinazohusiana
captcha