IQNA

Iran kuanzisha shule 1,200 mpya za kuhifadhi Qur’ani ndani ya miaka mitano

16:04 - May 11, 2025
Habari ID: 3480671
IQNA – Wizara ya Elimu ya Iran inapanga kuanzisha shule rasmi 1,200 mpya za kuhifadhi Qur’ani ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi.

Akizungumza na IQNA, Mikaeil Bagheri, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Qur’ani, Etrat na Sala katika wizara hiyo, amesema baadhi ya shule hizi tayari zinafanya kazi kwa majaribio.

Alibainisha kuwa shule hizi zitaanzishwa kwa mujibu wa Mpango wa Saba wa Maendeleo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akitilia mkazo umuhimu ambao Wizara ya Elimu inaupa ukuzaji wa hifadhi ya Qur’ani miongoni mwa wanafunzi wa shule, alisema: “Kama mnavyojua, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa muda mrefu amesisitiza kwamba tunapaswa kuwa na watu milioni 10 wanaohifadhi Qur’ani. Hivyo basi, Waziri wa Elimu amekuwa akisisitiza kwamba juhudi za dhati zichukuliwe katika nyanja ya kuhifadhi Qur’ani ili kufanikisha sehemu kubwa ya malengo ambayo bado hayajafikiwa.”

Aliongeza kuwa katika eneo la kuwaandaa wahifadhi wa Qur’ani, Wizara ya Elimu ni miongoni mwa taasisi zilizofanikiwa zaidi.

“Ikiwa taasisi zote zingekuwa na juhudi kama za Wizara ya Elimu katika uwanja huu, tungepiga hatua kubwa zaidi kwenye njia hii.”

Kwa mujibu wa Bagheri, utambuzi na uendelezaji wa vipaji vya Qur’ani pia ni kipaumbele cha juu kwa Waziri wa Elimu, ambaye anaamini kwamba hakuna mwanafunzi anayepaswa kubaki bila kufahamu kipaji chake au kukosa nafasi ya kukikuza kutokana na mapungufu ya mfumo wetu, hasa katika sekta ya Qur’ani.

“Kuhusu kutambua vipaji, kwa sasa tunaendesha mradi wa majaribio katika maeneo 16 ya kielimu nchini ili kutekeleza kazi hii mashuleni kwa kushirikiana na vituo vya Dar-ul-Qur’an pamoja na wataalamu wa kimataifa wa Qur’ani, ili tuweze kutambua vipaji kupitia msaada wa walimu, na zoezi hili litapanuliwa hatua kwa hatua hadi maeneo mengine ya kielimu.”

Amefafanua kuwa jukwaa kuu la elimu ya Qur’ani kwa ujumla ni shule, ilhali elimu ya kitaalamu zaidi hutolewa katika vituo vya Dar-ul-Qur’an.

Iran to Establish 1,200 Quran Memorization Schools in 5 Years

Wakati mwingine, endapo sekta ya elimu inachelewa kwa sababu yoyote, sehemu ya uwezo wa vituo vya Dar-ul-Qur’an hutumika pia katika kutoa elimu ya jumla ya Qur’ani, alieleza.

“Dira yetu ni kutekeleza programu za ziada za kielimu, na katika muktadha huu, kuna takriban vituo 860 vya Dar-ul-Qur’an vinavyofanya kazi kote nchini, vikihudumia viwango 10 vya kielimu , kuanzia usomaji wa msingi wa Qur’ani hadi mafunzo ya Sawt (sauti) na Lahn (melodi ya kisomo), vikihusisha elimu ya jumla na ya kitaalamu.”

Bagheri aliongeza kuwa elimu ya jumla ya Qur’ani inajengwa juu ya nguzo tatu: “Moja ni kitabu cha kiada, ya pili ni mwalimu, na ya tatu ni mwanafunzi. Ni muhimu sana kufundisha somo hili kwa njia ya kuvutia, tofauti na masomo mengine ambapo hata kama kitabu hakivutii, mzazi na mwanafunzi hujilazimisha kujifunza. Lakini katika Qur’ani, pamoja na maudhui sahihi ya kitaaluma, sura ya nje ya somo lazima pia ivutie.”

Aidha, alisema kuwa wenzake katika Taasisi ya Utafiti ya Wizara hiyo wanafanya kazi ya kuwasilisha vitabu vya Qur’ani vyenye muonekano tofauti, vinavyovutia na vyenye utofauti unaoendana na watoto, ili kuongeza hamasa ya wanafunzi katika kujifunza Qur’ani.

3493034

captcha