Mashindano hayo mashuhuri, ambayo tokea yaanzishwa yamekuwa na washiriki 2,107 kutoka nchi 91 kwa miaka yote, sasa yatatoa fursa ya washiriki kujisajili moja kwa moja, bila haja ya uteuzi rasmi wa nchi zao.
Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano, ilitangazwa kuwa jumla ya zawadi zitakuwa Dirham milioni 12, ikijumuisha zawadi ya kwanza ya dola milioni 1. Tuzo hii inaendelea kuimarisha nafasi ya Dubai kama kituo cha kimataifa cha ubora wa Qur’ani na elimu ya Kiislamu.
Mashindano yamefanyiwa mabadiliko makubwa kwa kurahisisha aina zake katika sehemu tatu kuu: Tuzo ya Wanaume, Tuzo ya Wanawake, na Tuzo ya Shakhsia wa Kiislamu wa Mwaka. Hatua hii ni hatua kubwa katika kupanua ushiriki na kuongeza athari ya tuzo hiyo kimataifa.
Washiriki lazima wawe na umri wa chini ya miaka 16 wakati wa kujisajili na wawe wamehifadhi Qur’ani nzima kwa usahihi pamoja na sheria za Tajweed. Wale ambao wamefika fainali au kupata zawadi katika matoleo yaliyopita hawataruhusiwa kushiriki tena.
Usajili wa vipengele vya wanaume na wanawake utafunguliwa kuanzia Mei 21 hadi Julai 20, 2025, kupitia tovuti rasmi ambayo ni www.quran.gov.ae
Tathmini ya awali itafanyika kati ya Julai 1-31, ikifuatiwa na hatua ya pili ya majaji kupitia video kati ya Septemba 1-30.
Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai ilianzishwa mnamo 1997 kwa agizo la Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa UAE, ambaye pia ni Mtawala wa Dubai.
3493187