Haya ni kwa mujibu wa Majid Namjoo, afisa wa kuandaa mawkib katika Makao Makuu ya Iran ya Arobaini ya Imam Hussein (AS). Alitoa kauli hizo alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari siku ya Jumatatu kuhusu matembezi ya Arbaeen.
Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu). Kando ya njia ya matembezi ya Arbaeen, mawkib huanzishwa ili kutoa malazi, huduma za afya, masaji ya mwili na miguu, na ukarabati wa zana. Neno hili limekuwa likitumika sana katika utamaduni wa Mashia wa Iraq.
Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).
Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi ya wasiokuwa Mashia humiminika Karbala, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala.
3489219