IQNA

Arbaeen 1446

Arbaeen: Mawkib kwenye Barabara ya Najaf-Karbala

15:09 - August 19, 2024
Habari ID: 3479301
IQNA – Jumba la Makumbusho la Al-Kafeel, lenye mafungamano na Haram Takatifu ya Hazrat Abbas (AS), limeweka Mawkib kwenye barabara ya Najaf-Karbala ili kuwahudumia wafanyaziara wa Arbaeen.

Kwa mujibu wa jumba hilo la makumbusho, mpango huo unalenga kuongeza ufahamu wa kitamaduni na kielimu kupitia shughuli mbalimbali, zikiwemo programu za Qur'ani, semina za kitamaduni, mihadhara ya kidini, maonyesho ya vitabu, programu za simu na mashindano.

Sadegh Lazem-Zaidi, afisa wa jumba la makumbusho, alieleza kuwa moukeb inaonyesha nakala za vitu vya thamani na nguo zilizotengenezwa kwa mikono huku pia ikitoa mahali pazuri pa kupumzika kwa washiriki wa maandamano ya Arbaeen.

Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) na kupata sehemu ya kupumzika na malazi.

Mjumuiko wa maombolezo ya Arbaeen ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

3489555

 

Habari zinazohusiana
captcha