IQNA

Arbaeen 1446

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa na familia zao kuhudhuria Arbaeen

11:24 - August 11, 2024
Habari ID: 3479261
IQNA - Afisa wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (SAW) anasema maelfu ya wanafunzi kutoka chuo hicho watashiriki matembezi ya Arbaeen mwaka huu ili kueneza mafundisho ya Kiislamu.

Wanafunzi 20,000 na familia zao watashiriki katika matembezi  ya mwaka huu ya Arbaeen, Hujjatul Islam Majid Khaleghpour, naibu mkuu wa chuo kikuu, alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi. Alibainisha kuwa msafara wa kwanza ulianza safari ya kiroho siku ya Ijumaa.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdii na jeshi la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi ya wasiokuwa Mashia humiminika Karbala, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala.

Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.

3489454

Habari zinazohusiana
captcha