Semina hii ni miongoni mwa mfululizo wa matukio ya kila wiki ya tafsir ya Qur’an yanayoandaliwa ndani ya Msikiti huo maarufu wa Al-Azhar.
Wale wanaoohudhuria ni pamoja na Ustadha Hamdi al-Hudhud, mkuu wa shule ya wasichana ya ‘Al-Asher Min Ramadan’ , mojawapo ya miji mipya ya Misri inayosimamiwa na Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na pia Profesa Mustafa Ibrahim kutoka Kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar.
Sheikh Abdul Munim Fuad, msimamizi mkuu wa shughuli za kielimu za Msikiti wa Al-Azhar, alisema kuwa semina hii ni fursa muhimu ya kutafakari aya za Qur’an Tukufu na kuelewa maana zake kwa undani zaidi. Aliongeza kuwa ni njia ya kufungua milango mipya ya utafiti kuhusu miujiza ya kisayansi ndani ya Kitabu Kitukufu.
Alieleza kuwa mkutano huu utasaidia sana katika kukuza uelewa wa kidini na kitamaduni kwa washiriki, pamoja na kuwatia moyo kutafakari kwa kina maandiko ya Kiislamu.
Sheikh Hani Awdah, msimamizi wa Msikiti wa Al-Azhar, alionesha kuridhishwa na uandalizi wa semina hii, akisisitiza umuhimu wa miujiza ya Qur’an katika kujenga utambulisho wa Umma wa Kiislamu (Ummah). Alisema kuwa Msikiti wa Al-Azhar umejikita katika kukuza elimu kwa lengo la kuijenga jamii yenye uelewa na utamaduni wa Kiislamu, na kuwa semina za tafsir ni sehemu ya mpango mpya kufanikisha malengo hayo.
Awdah alieleza kuwa semina za tafsir ya Qur’an Tukufu hufanyika mara kwa mara kila Jumapili, zikihudhuriwa na wanazuoni na maprofesa kutoka Al-Azhar. Aliongeza kuwa sehemu ya semina hiyo imetengwa kwa ajili ya maswali na majadiliano ya wazi, yatakayowapa washiriki fursa ya kubadilishana mawazo na kueleza mitazamo yao.
Ni vyema kutambua kuwa katika Qur’an Tukufu, upepo umetajwa kama miongoni mwa alama za uweza wa Mwenyezi Mungu. Aya mbalimbali za Kitabu Kitukufu zinaonyesha mchango wa upepo katika kuchochea mawingu, kuyasukuma, kuelekeza katika pande tofauti, na athari zake katika maisha. Qur’an Tukufu inataja upepo kama lawaqih (vichochezi) vinavyofanya mbolea ya mawingu na kusababisha mvua kunyesha.
Vilevile, Qur’an inatumia kauli ya “Tasrif al-Riyah” kumaanisha mabadiliko ya mwelekeo na kasi ya upepo, ikionesha kuwa Mwenyezi Mungu anauendesha upepo kulingana na maslahi na mahitaji ya binadamu.
Qur’an pia imetambua upepo kuwa ni rahma (rehema) kutoka kwa Allah, lakini pia unaweza kuwa ni adhabu kama vile upepo wa sumu au dhoruba kali.
3493819