IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Mtihani waanza kwa wahifadhi Qur'ani wanaotaka Kujiunga na Al-Azhar

20:47 - January 17, 2023
Habari ID: 3476419
TEHRAN (IQNA) – Mtihani wa nne wa kuchagua wahifadhi Qur’ani wanaotaka kujiunga na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri umeancha nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Akhbar al-Yawm, wahifadhi Qur'ani kutoka majimbo yote ya Misri wanafanya mtihani huo katika Msikiti Mkuu wa Al-Azhar.

Mtihani huo ulianza  Jumatatu, Januari 16 na utaendelea kwa siku tatu.

Kisha kamati itachagua wahifadhi ambao watajiunga na Al-Azhar kulingana na alama zao katika mtihani.

Kamati hiyo inaongozwa na Abdul Karim Saleh na Sheikh Hassan Abdul Nabi Araqi ndiye naibu mkuu wake.

Mkurugenzi wa Msikiti wa Al-Azhar Hadi Awda alisema mtihani huo unafanyika kwa kutumia vifaa bora ili kuhakikisha kunakuwepo uadilifu katika tathmini na watahiniwa wote watapata fursa sawa.

Mtihani huo huandaliwa kila mwaka kwa amri ya mkuu wa Al-Azhar ambaye kwa sasa ni Sheikh Ahmed El-Tayeb.

4115232

captcha