IQNA

Harakati za Qur'ani

Al-Azhar kuandaa warsha kwa waamuzi wa Mashindano ya Qur'ani Tukufu

21:01 - February 08, 2023
Habari ID: 3476534
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kinatarajia kufanya warsha maalum wiki ijayo kwa waamuzi au majaji katika mashindano ya Qur'ani Tukufu.

Warsha hiyo itazingatia vigezo na taratibu za kuhukumu mashindano ya Qur'ani Tukufu nchi nzima ambayo yanaandaliwa na kituo hicho.

Washiriki wanatayarishwa kuwa majaji wa mashindano ya Qur'ani Tukufu.  Kulingana na Al-Azhar, washiriki 59,495 wamefanikiwa kuingia hatua inayofuata ya hafla hiyo ambayo itaanza mnamo Februari 25.

Majaji watafunzwa kutumia  mfumo wa kielektroniki kuainisha alama kwani Al-Azhar inatumai kuwa mbinu kama hiyo itaondoa makosa ya mbinu za kijadi.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani Tukufu ni za kawaida sana katika nchi ya Kiarabu yenye Waislamu wengi. Misri ni nchi yenye wasomaji Qur'ani Tukufu.

4120549

4101564

4120549

captcha