Huu ni mpango maalum wa Qur'ani kwa vituo vinavyohusiana na Al-Azhar na vituo vyote binafsi vya kuhifadhi Qur'ani nchini Misri ambavyo vinafanya kazi chini ya usimamizi wa Al-Azhar.
Mpango huu wa Qur'ani kwa majira ya joto ulianza leo na utaendelea hadi Agosti 31, 2025.
Kwa mujibu wa idara kuu ya masuala ya Qur'ani ya vituo vinavyohusiana na Al-Azhar, washiriki watafundishwa kuhifadhi Qur'ani bila malipo kupitia mbinu mbili.
Mbinu ya kwanza inaitwa “Hifadhi ulichoainishiwa”, inayotekelezwa katika vituo vya Al-Azhar siku tatu kwa wiki kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 adhuhuri.
Mbinu ya pili inaitwa “Duru 10,000 za Qur'ani”, inayotekelezwa katika vituo binafsi vya kuhifadhi Qur'ani vinavyofanya kazi chini ya usimamizi wa Al-Azhar.
Mpango huu wa Qur'ani wa majira ya joto unatekelezwa kwa msaada wa Mkuu wa Al-Azhar, Sheikh Ahmed Al-Tayeb.
Mkurugenzi Mkuu wa Vituo Vinavyohusiana na Al-Azhar pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Qur'ani wa Al-Azhar watausimamia mpango huu.
3493292