IQNA

Uislamu nchini Morocco

Morocco yatenga dola milioni 192 kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi ya Maimamu

12:53 - June 23, 2022
Habari ID: 3475416
TEHRAN (IQNA) – Mpango wa usaidizi unaolenga kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi ya maimamu wanaosalisha misikitini kote nchini Morocco utatekelezwa nchini humo.

Akijibu maswali ya Wabunge Jumanne, Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Morocco Ahmed Toufiq alisema kuwa wizara hiyo imetenga bajeti inayokadiriwa kuwa ya dola milioni 192 kuboresha hali za maimamu.

Alisema bajeti hiyo itajumuisha marupurupu ya  kila mwezi, huduma ya afya na mafunzo.

Kiwango cha chini cha marupurupu kimongezwa na kufika kati ya dola 228.85 hadi dola 258.70  kwa maimamu na kati ya dola 248.75 hadi  dola 368.15 kwa wanaofanya kazi za maeneo mengine ya kawaida mbali kuhudu kama maimamu.

Toufiq alibainisha kuwa maimamu wamekuwa na uwezo wa kufikia mfumo wa huduma ya afya tangu 2007.

"Upatikanaji wa huduma za afya umefanywa kwa ujumla katika 2014 kwa wafanyakazi wote wa kidini, ikiwa ni pamoja na wahubiri na wakaguzi wa misikiti," waziri aliripoti.

Toufiq alisema kuwa mfumo wa huduma ya afya unanufaika kutokana na bajeti ya kila mwaka inayokadiriwa kufikia  dola milioni 22.86.

Toufiq pia alijibu maswali kuhusu misikiti na kusema  tangu 2011, Morocco ilikarabati misikiti 1,382 kati ya 3,665 kwa bajeti ya karibu  dola milioni 238.8 milioni.

Licha ya juhudi hizo, waziri alidokeza kuwa kuna misikiti 1,225 ambayo inahitaji ukarabati kwa bajeti inayokadiriwa kufikia  dola milioni $199 milioni.

Morocco ina misikiti inayokadiriwa kuwa takribani 50,000.

3479425

Kishikizo: Morocco ، Morocco ، maimamu ، toufiq
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :