
Waandamanaji wenye mitazamo tofauti walibishana na kusukumana mitaani Novemba 18, wakijadili dini na uhamiaji, huku baadhi wakitoa wito wa mshikamano.
Kulikuwa na madai ya matumizi ya dawa ya pilipili (pepper spray), lakini kwa ujumla hakukuwa na matukio makubwa ya madhara. Polisi wa Dearborn walitoa taarifa Jumanne jioni, wakiwataka wananchi kuepuka kujibizana na waandamanaji waliotoa kauli za chuki dhidi ya Uislamu, wahamiaji na wachache.
Kufikia saa 12 jioni, umati uliongezeka ukimkabili Jake Lang, mwanaharakati wa mrengo wa kulia kutoka Florida aliyepanga moja ya mikutano mitatu ya siku hiyo. Polisi waliweka vizuizi vya chuma kuwatenganisha Lang na wafuasi wake na umati uliokuwa ukimshutumu.
Afisa Bartok alisema kulikuwa na “matukio madogo mapema mchana” lakini hakukuwa na tishio kubwa kwa usalama wa umma.
Mwanaharakati Hudson alikiri awali alidhani Dearborn imechukuliwa na Waislamu kwa kutekeleza sheria ya Sharia, lakini baada ya kutembelea misikiti minne na biashara kadhaa, alibaini si kweli.
Kabla ya mkutano, Lang alitangaza kuwa angechoma nakala ya Qur'ani Tukufu na kukaanga nyama ya nguruwe, lakini kufikia saa 12 jioni hakufanikisha lengo lake. Wakati fulani alinyanyua nakala ya Qur'ani akiwa na chupa ya mafuta ya kuwasha moto na kutoa maneno ya dharau dhidi ya Mtume Mtukufu (SAW). Alipoiweka Qur'ani chini na kujaribu kuichoma, Mwislamu mmoja aliyeandamana akamnyang’anya kitabu hicho. Baadaye, Lang alitoa kipande cha nyama ya nguruwe na kuipiga Qur'ani nacho katikati ya barabara ya Michigan Avenue, lakini tena Mwislamu mwingine akamnyang’anya kitabu hicho.
3495450