IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washiriki wa kike katika Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran wazawadiwa

17:57 - December 09, 2024
Habari ID: 3479883
IQNA - Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Iran yalihitimisha sehemu zake za wanawake na wasichana chini ya umri wa miaka 18 kwa  sherehe huko Tabriz, zilizofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 9 Disemba.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Wakfu na Misaada Iran, iliwaleta pamoja wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani wenye vipaji vya hali ya juu zaidi kutoka kutoka kote Iran

Azarman Sadeghi kutoka Tehran alitajwa kuwa mshindi wa kitengo cha usomaji wa Qur'ani. Asieh Dehghan kutoka Mkoa wa Fars na Zeinab Khazalizadeh kutoka Mkoa wa Khuzestan walishika nafasi zilizofuata.

Katika kuhifadhi Qur'ani nzima, Zahra Ansari kutoka Tehran alipata zawadi ya kwanza. Majideh Rezapour kutoka Mkoa wa Kerman na Fatemeh Ebrahimi kutoka Mkoa wa Fars walifuata..

Washindi wakuu wa kategoria nyingine, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Tarteel, kuhifadhi Juzuu20, kuhifadhi Qur'ani nzima kwa wasichana wenye umri wa chini ya miaka 18, na usomaji wa Qur'ani kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18, pia walitunukiwa katika sherehe hizo.

Mashindano hayo ya kila mwaka, yanayochukuliwa kuwa mashuhuri zaidi ya Qur'ani nchini Iran, yanalenga kukuza maadili ya Kiislamu, kukuza ujuzi wa kusoma na kuhifadhi Qur'ani, na kusherehekea vipaji vya kipekee.

Sehemu ya shindano la wanaume imepangwa kuanza  katika mji huo wa Tabriz mnamo Desemba 10.

Washindi wakuu wa mashindano hayo wataiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kote duniani.

4252994

captcha