IQNA

Wananchi wa Iran wapiga kura katika uchaguzi wa rais

13:58 - June 19, 2021
Habari ID: 3474019
TEHRAN (IQNA)- Mamilioni ya wananchi wa Iran jana walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa rais na pia uchaguzi wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji.

Zoezi la kupiga kura lilimalizika Jumamosi (Juni 19) saa nane usiku, masaa 19 baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa saa moja asubuhi Ijumaa, Juni 18.

Muda wa zoezi la kupiga kura uliongezwa mara kadhaa ili kuhudumia idadi kubwa ya wapiga kura na pia kutokana na uzingatiaji wa kanuni za kiafya za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Zaidi ya Wairani milioni 59 walikuwa wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi ambao ulikuwa wa wagombea wanne baada ya Wagombea wengine watatu kujiondoa katika mchuano huo Jumatano.

 
 
Kishikizo: uchaguzi ، iran
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha