IQNA

Arbaeen 1446

Waziri Mkuu: Iraq inatazamia wafanyaziara milioni 23 washiriki Arbaeen ya Imam Hussein (AS)

13:33 - August 18, 2024
Habari ID: 3479294
IQNA - Waziri Mkuu wa Iraq alisema idadi ya wafanyaziara wa Arbaeen kutoka Iraq na nje ya nchi inatarajiwa kufikia milioni 23 mwaka huu.

Mohammed Shia' Al Sudani alisema hayo alipotembelea chumba cha operesheni cha wizara ya mambo ya ndani, tovuti ya habari ya al-Maluma iliripoti.

Wakati wa ziara hiyo, alifahamishwa kuhusu mpango wa usalama uliopo kwa msimu wa Arbaeen.

Waziri Mkuu alishukuru vikosi vya usalama na jeshi kwa juhudi zao za kuhakikisha usalama wa wafanyaziara.

Al Sudani amesema kwa kuwa idadi ya wafanyaziara wa Arbaeen kutoka maeneo tofauti ya Iraq na nchi nyingine inatarajiwa kuzidi milioni 23 mwaka huu na kuongeza kuwa juhudi zinapaswa kufanywa ili kurahisisha shughuli hii ya kidini

Alisema wafanyaziara 140,000 wa Arbaeen huingia Iraq kila siku kutoka nje ya nchi ambapo ameshukuru zaidi juhudi kwa wale wanaoendesha Mawkib ambao amesema wamesaidia mashirika ya usalama na watoa huduma.

Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) na sehemu ya kupumzika.

Mjumuiko wa maombolezo ya Arbaeen ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

3489531

Habari zinazohusiana
Kishikizo: shia al sudani arbaeen
captcha