Katika sherehe ya kuwaenzi wahifadhi 1,000 wa kiume na wa kike wa Qur’ani iliyofanyika Jumamosi, Spika wa Bunge, Mahmoud Al-Mashhadani, alitangaza mpango huo, akisisitiza jukumu muhimu ambalo waifadhi Qur’ani wanalo katika kuhifadhi maadili ya kidini.
“Wahifadhi hawa ni walinzi wa maarifa na vitendo. Wanapaswa kuwa mfano wa uaminifu na ukarimu kwa sababu Qur’ani inalea roho na inaboresha tabia,” Al-Mashhadani alisema wakati wa tukio hilo, kama ilivyoripotiwa na Alsumaria News.
Alisisitiza dhamira ya Bunge ya kuandaa sheria inayolenga kuhakikisha haki za wahifadhi wa Qur’ani, akiwapongeza kwa jukumu lao katika kueneza mafunzo ya Kiislamu na kukuza viwango vya juu vya maadili.
Al-Mashhadani alielezea sherehe ya kuhitimu kwa wahifadhi 1,000 wa Qur’ani kama “ushahidi wa uhai wa taifa la Kiislamu” na aliwasifu waheshimiwa hao kama “walinzi wa amana kubwa na chanzo cha fakhari kwa kila mtu.”
Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia’ Al-Sudani, ambaye aliwapongeza washiriki na kupongeza mpango wa “Hafidh Rabbani”.
Mpango huu wa kitaifa uliyozinduliwa hivi karibuni unalenga kuhamasisha kuhifadhi Qur’ani na kukuza maadili ya Kiislamu kote Iraq.
3491266