Vituo vya kupigia kura vILIfunguliwa mapema saa mbili asubuhi kwa majira ya hapa Iran huku Tume ya Uchaguzi ikitangaza kuwa, maafisa wake wamejiandaa kikamilifu kuendesha zoezi la uchaguzi huu.
Wairani wasiopungua milioni 61 wametimiza masharti ya kupiga kura. Wagombea wanne wanatarajiwa kuchuana kuwania kiti cha Urais ambao ni Saeed Jalili, mkuu wa zamani wa timu ya mazungumzo ya nyuklia, Muhammad Bagher Qalibaf, spika wa Bunge la Iran, Mostafa Pourmohammadi, waziri wa zamani wa mambo ya ndani na Masoud Pezeshkian, waziri wa zamani wa afya. Wagombea wawili Alireza Zakani, meya wa jiji la Tehran na Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi mkuu wa Wakfu wa Mashahidi na Masuala ya Veterani jana walitangaza kujitoa katika mbio za kuwania urais. Duru mbalimbali zinatabiri kuwa, ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa kati ya wagombea watatu ambao ni Saeed Jalili, Muhanmmad Bagher Qalibaf wa mrengo wa wahafidhina na Masoud Pezeshkian wa mrengo wa wapigania mageuzi.
Kiongozi Muadhamu
Wakati huo huo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka wananchi wa Iran kutosita hata kidogo kushiriki katika uchaguzi wa leo wa Rais.
Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alipiga kura yake katika sanduku la kupigia kura leo Ijumaa asubuhi wakati wa kuanza zoezi la upigajii kura wa duru ya 14 ya uchaguzi wa Rais, ambapo amepiga kuura yake katika kituo cha kupigia kura cha Husseiniya ya Imam Khomeini.
Baada ya kupiga kura yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja siku ya uchaguzi kuwa siku ya furaha na nishati kwa Wairani na kuashiria uthabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia ushiriki wa wananchi katika uchaguzi. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: Wananchi wapendwa wa Iran, suala la kupiga kura na kushiriki katika mtihani huu muhimu wa kisiasa lichukulieni kwa uzito jambo hili na msiruhusu hali yoyote ya shaka na kusitasita iingie katika nafsi zenu.
Muda wa kupiga kura waongezwa
Msemaji wa Tume ya Uchaguzi nchini Iran amewaambia waandishi wa habari kwamba, muda wa kupiga kura katika uchaguzi wa rais ulioanza mapema leo kote nchini umerefushwa kwa saa 2, yaani hadi saa mbili usiku.
Mohammad Eslami, msemaji amewaambia waandishi wa habari kwamba, kwa idhini ya Waziri wa Mambo ya Ndani Ahmed Vahidi, muda wa kupiga kura katika uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu umerefushwa kwa saa 2, hadi saa mbili usiku.
Duru ya 14 ya uchaguzi wa rais ilianza saa mbili kamili asubuhi Ijumaa ya leo - Julai 8 - katika vituo 58,640 vya kupigia kura kote nchini Iran.
Vilevile, vituo 344 vya kupigia kura vilitayarishwa katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya Wairani wanaoishi ng'ambo ili kumchagua Rais wa Serikali ya Awamu ya 14 katika balozi na vituo vya uwakilishi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi nyingine.
3488911