IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Iran yawataja wawakilishi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi

10:04 - December 21, 2023
Habari ID: 3478069
IQNA - Wawakilishi wa Iran katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa wanafunzi wa shule walitangazwa.

Naibu waziri wa elimu na mkurugenzi wa idara ya Qur'ani Tukufu, Etrat na Sala ya wizara hiyo Mikaeil Baqeri alisema wamechaguliwa baada ya kushinda nafasi za juu katika mashindano ya kufuzu yaliyofanyika wiki hii kwenye kambi ya Shahid Bahonar mjini Tehran.

Amesema Mehdi Akbari Zarrin kutoka Mkoa wa Qom na Seyed Mohammad Sadeq Hosseini Razavi Mkoa wa Khorasan wataiwakili9sha Iran katika kategoria za qiraa na hifdhi, sehemu ya wavulana.

Katika sehemu ya wasichana, Asma Falaki kutoka Razavi Khorasan na Mohanna Qanari kutoka Gilan watawakilisha Iran, alisema.

Toleo la 8 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa wanafunzi wa shule yamepangwa kufanyika nchini Iran mapema mwaka 2024.

Baqeri alibainisha zaidi kwamba Bangladesh imetuma mwaliko kwa Iran kwa ajili ya kumtambulisha mwakilishi wake, mwenye umri wa chini ya miaka 16, kushindana katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya nchi hiyo ya Kusini mwa Asia.

Hivyo, aliongeza, Amir Hadi Bairami kutoka Mkoa wa Ardebil atatumwa kwenye mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu nchini Bangladesh.

8000985

Habari zinazohusiana
captcha