IQNA

Wanafunzi Waafrika Karbala, Iraq wapata mafunzo maalumu ya Qur'ani

15:53 - July 01, 2021
Habari ID: 3474060
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS huko Karbala, Iraq imeandaa warsha ya qiraa ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya wanafunzi Waafrika wanaosoma katika vyuo vya Kiislamu (Hawza) mjini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kituo cha Kufunza Qur'ani cha Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS kimetoa mafunzo hayo kwa ushirikiano na Kituo cha Wanafunzi wa Afrika cha idara hiyo.

Hii ni duru ya pili ya warsha hiyo ya Qur'ani ambayo imepewa jina la 'Imam Hassan Mujtaba AS'.

Kuwafunza wanafunzi qiraa sahihi ya Qur'ani Tukufu ni lengo kuu la warsha hiyo. Wanafunzi 30 kutoka nchi mbali mbali za Afrika  walioko mjini Karbala watapata mafunzo katika kipindi cha miezi miwili.

Mafunzo hayo yanasimamiwa na Alauddin al Humairy, ambayo ni mkuu  wa qiraa ya Qurani Tukufu katika Kituo cha Kufunza Qur'ani cha Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS.

 
captcha