IQNA

Nakala za Qur’ani Tukufu zachomwa moto Msikitini nchini Italia

20:47 - March 19, 2014
Habari ID: 1389037
Kundi la watu wasiojulikana limeushambulia msikiti mmoja kaskazini mwa Rome mji mkuu wa Italia na kuteketeza nakala zote za Qur’ani Tukufu zilizokuwemo msikitini humo.

Kwa mujibu  wa mwandishi wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA,Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu nchini Italia Sha'ab al Jadid amelaani shambulio hilo na kuitaka serikali ya Rome kuzuia vitendo vinavyoyavunjia heshima matukufu ya dini ya Kiislamu na Waislamu kwa ujumla. Jumuiya hiyo inasimamia misikiti ipatayo 250 nchini Italia.

Ijapokuwa nchi za Ulaya daima zimekuwa zikijinadi kuwa mstari wa mbele katika kuchunga misingi ya haki za binadamu na uhuru wa kuabudu, lakini haziko tayari kuona Uislamu ukizidi kupata nguvu barani humo. Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, wahajiri Waislamu wanaoishi katika nchi za Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Italia mara kwa mara wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kibaguzi vinavyofanywa na wenyeji na wazawa wa nchi hizo.

1388920

Kishikizo: italia qur'ani nakala moto
captcha