IQNA

Uturuki kusambaza Misahafu milioni moja Afrika

14:38 - July 13, 2015
Habari ID: 3327631
Taasisi mbili za Uturuki zinashirikiana kusambaza nakala milioni za Qur’ani Tukufu katika nchi kadhaa za Kiafrika.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mradi huo unatekelezwa na Shirika la Ushirikiano la Uturuki na Shirika la Misaada la Hayarat pia la Uturuki.
Mwenyekiti wa Shirika la Misaada la Hayrat Hakkı Akgün akizungumza nchini Sudan wakati wa kukabidhi nakala 50,000 za Qur’ani alisema misahafu hiyo imechapishwa nchini Uturuki. Ameongeza kuwa nakala hizo milioni moja za Qur’ani zitasambazwa Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Ameongeza kuwa, shirika la Hayrat halitoa tu misaada ya kibinadamu bali pia linajihusisha na  msuala ya utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu.
Naye Yahya Acu Shirika la Ushirikiano la Uturuki amesema wanajitahidi kuimarisha uhusiano wa Uturuki na nchi ambazo wanaendesha harakati za maendeleo.../mh

3327374

captcha